Malengo ya Watoto App ni mradi wenye lengo la kuwajengea Uelewa wazazi na walezi wa watoto kuhusiana na malezi bora ya watoto nchini Tanzania na dunia kiujumla. Mradi huu ulianzishwa 5 February 2020 kupitia Android Application (App) inayopatikana google play store kwa jina Malezi ya Watoto App.Ikiwa na dhima kubwa ya kulinda na kutetea haki na maslahi ya watoto kwa jamii.

 Lengo kuu/Dira (Our vision)

Kuunganisha mipango na juhudi za kukabiliana na kuondoa Ukatili dhidi ya watoto ili uwe mfumo wa jamii unaofanya kazi.

 Dhima (Our mission)

Kumlinda mtoto wa Tanzania na dunia kiujumla.

 Kazi zetu za msingi (Our core function)

  • Kufundisha na kutoa Mafunzo kuhusu malezi bora ya watoto na kuwalinda watoto dhidi ya matukio ya ukatili.
  • Kuzuia matukio ya ukatili dhidi ya watoto kwa kutoa Elimu kinga Kwa wanajamii.
  •  Kufanya utafiti na kutoa unasihi na ushauri kuhusiana na malezi bora ya watoto kwa jamii.
  • Kukusanya na kuweka kumbukumbu za matukio ya ukatili dhidi ya watoto.
  • Kutumia kumbukumbu za matukio ya ukatili dhidi ya watoto ili kuepusha matukio mengine yasitokee siku zijazo.
  • Kuchunguza na kubaini aina za Ukatili dhidi ya watoto katika jamii.
  • Kutoa taarifa za Ukatili dhidi ya watoto kwa jamii.
  • Kuunganisha na kukutanisha wazazi na walezi wa watoto kujadiliana masuala ya malezi bora ya watoto.