Malezi bora ya Watoto ni hatua ya kwanza katika kujenga Taifa lenye kizazi bora na Msingi mzuri wa Maendeleo ya Watu wa Taifa husika.
Watoto ni taifa la kesho, Kwa Msingi huo Malezi ya Watoto ni jukumu la Taifa zima. Taifa Imara na lenye watu wenye Akili nzuri na Afya bora hutokana na watoto waliozaliwa na kulelewa katika mazingira yanayofaa.
Kwa Tanzania na Afrika kiujumla Matatizo ya Malezi kwa watoto wetu ni makubwa sana, Baadhi yake yapo chini ya uwezo wetu, Matatizo haya husababishwa na baadhi ya wanajamii wenyewe kwa sababu hawajayapa kipaumbele Masuala yote yanayohusu ufumbuzi wa Matatizo na Maendeleo ya Mtoto katika Elimu, Mavazi, Chakula na Mambo mingineyo ya muhimu kwa Watoto.